Bambara

Kasonke

Castellano

Magyar

Català

Swahili

Deutsch

Português

English

Română

Français

Türkçe

Aktuell: Theateraufführung am Samstag, 23. September 2017

 

Wir spielen unser Stück "What's the difference?", in dem es um Rollenklischees im Alltag geht- ob am Arbeitsplatz, in der Familie oder im Einkaufszentrum.
 
 WANN? 23. September 2017, 19 Uhr
 WO? Spektakel Theater, Hamburgerstrasse 14, 1050 Wien
 Eintritt: freie Spende

Sisi ni nani…

Spiegel dich! ni kundi la watu vijana wasio na utaalamu. Msingi wa kundi umetoka katika wazo, kuwa “Kila mtu anaweza kuigiza tamthilia!” Kundi letu lilianza kama mradi kwa tasnifu ya digrii moja iliyoandikwa wakati wa majiora ya kipupwe 2010 na limezidi kuongezeka. Spiegel dich! ni kundi la watu tofauti: Tunatoka katika nchi tofauti na tunasoma lugha tofauti. Kila mjumbe ana namna yake ya kuwasiliana, anayo njia yake katika kusuluhisha mgorogoro namna na pia anao uwezo mkubwa anaoweza kuwafundisha wajumbe wengine. Kwa hiyo kauli mbiu yetu ni “Pamoja tuna utaalamu mkubwa!”

Tunafanya nini …

Katika kazi zetu tunatafuta uwezekano wa kusuluhisha migorogoro binafsi. Badala ya kuendelea na taratibu thabiti, tunajaribu mbinu tofauti za kusuluhisha migorogoro. Mpaka sasa tumetumia nadharia na mbinu za Schulz von Thun, Augusto Boal, J.P. Lederach na Marshall B. Rosenberg. Tumezungumza juu ya nadharia, tumejaribu mbinu tofauti za ‘Theatre of the Oppressed’ na tumechanganua mada bila kutumia nguvu.

Sababu gani tunaitwa ‚Spiegel dich!’ [Akisika!]?

Tunaleta tofauti zetu za kihistoria katika tamthilia, kwa sababu kuna uwezekano mkubwa zaidi. Wakati huo huo mjumbe mmoja anamwakisi mwingine: Sisi ni vioo kwa wengine. Hivyo tunaweza kuonana kwa namna nyingine, kama tukiweza kujikosoa wenyewe.

 

Maana ya ‚Spiel dich!’ [Jaribu!] ni kwamba tunatumia michezo kama mbinu kwa kujaribu mandhari mbalimbali. Vilevile tunatoa wito wa kuvuka mipaka kwa mawazo mapya kupitia michezo na bila shaka.